Programu za Vijana na Watoto

Parokia Teule ya Mt. Monica imeweka mikakati na mipango mbali mabali katika kuhakikisha inawaleta vijana na watoto karibu na Mungu. Kama Parokia tunaamini kwamba vijana na watoto ndiyo nguvu kubwa ya kanisa kwa kizazi cha sasa na cha kesho pia na kama watatumika vyema watakuwa mabalozi wazuri wa Kristo kwa jamii ya kitaifa na kimataifa, na katika kuhakikisha hilo linafanikiwa Parokia imefanikiwa kuanzisha programu mbali mbali za makundi haya kama ifuatavyo.

PROGRAMU ZA WATOTO
Kwa upande wa watoto Parokia teule imefanikiwa kuanzisha JNNK za watoto katika kila jumuiya ndani ya Parokia Teule ambapo kila jumapili jioni hukutana na walezi wao na kupata mafundisho ya namna ya kuwa Wakristo bora na raia waaminifu

Pia Parokia Teule imeanzisha kwaya ya watoto ambayo hutoa huduma katika Ibada ya watoto kila Jumapili, kwaya hiyo ipo chini ya usimamizi wa Mt. Yohane Bosco na Padre Kiongozi wa Parokia ndiyo mlezi wa kwaya hiyo.  

Watoto wote hukusanyika kila jumamosi katika viwanja vya Parokia Teule kuanzia saa 2 : 00 Asubuhi mpaka saa 6 : 30 Mchana wakipokea mafundisho ya Katekismu kutoka kwa Katekista, Sista au Mafrateri katika maandalizi ya kupokea Komunio ya kwanza na Kipaimara.

Katika kuwaimarisha watoto wamekuwa na utaratibu wa kutembelea na Kufanya hija katika Parokia, Parokia Teule na Vigango mbali mbali vilivyopo ndani ya Jimbo la Moshi katika kujenga ushirikiano na kushirikishana yale amabayo wamekuwa wakifundishwa na waalimu wao wa kiroho.

PROGRAMU ZA VIJANA
Parokia Teule ya Mt. Monica imefanikiwa katika kuwaweka vijana karibu kwa kuwa na semina mbali mbali kila jumapili mara baada ya Misa ya pili na semina hizo huongozwa na Salesian Brothers of Don Bosco kwa kushirikiana na Uongozi wa umoja wa vijana Parokia (VIWAWA)

Pia Parokia Teule ya Mt. Monica Imefanikiwa katika kuanzisha na kuiendeleza kwaya ya vijana amabayo hutoa Huduma kwenye Ibada ya Pili kila jumapili, kwaya hii imekuwa kioo, kielelezo na chachu kwa vijana wengine kuhudhuria ibada wakishirikiana kwa karibu na kwaya za watu wazima za Mt. Agustino na Mt. Karoli Lwanga. Kwaya hii ya vijana imefanikiwa kutoa albamu yake moja inayokwenda kwa jina la MSAMAHA MSALABANI. Na pia wimbo Maalumu kwa ajili ya mwezi wa Rozari unaokwenda kwa jina la Mwezi wa Maria na unapatikana katika Youtube

PROGRAM ZA MUZIKI MTAKATIFU
Parokia Teule ya Mtakatifu Monica inajivunia mwamko wa vijana na watoto katika kujifunza muziki mtakatifu wa kikatoli ambapo hadi hivi sasa tuna waalimu watoto wawili wenye uwezo wa kucheza kinanda kwa ufasaha kabisa kwa nyimbo za ibada nzima. Pia tunaye kijana mmoja ambaye ni mwalimu mwanafunzi kutoka kwaya ya vijana mwenye uwezo wa kufundisha muziki wa noti na kucheza kinanda pia. Haya ni mafanikio na chachu inayoongeza shahuku ya Parokia Teule kuanzisha mchakato wa mafunzo ya Elimu ya muziki Mt. wa Kikatoli .